Loading...
company_logo

PDF YA WANAOITWA KWENYE INTERVIEW TRA

Sept. 16, 2023

TANGAZO

TRA inapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuanzia tarehe 27 Mei 2023 mpaka 09 Juni, 2023 kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kwa hatua mbalimbali kuanzia tarehe 24 September, 2023 na hatimaye kuwapatia barua ya ajira waombaji kazi watakaofaulu. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo: -

1. Usaili utafanyika kama ilivyooneshwa kwenye ratiba ikianisha siku, muda na sehemu.

2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.

3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: - Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au Hati ya kusafiria.

4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia Cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.

5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.

7. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili. 8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA).

9. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo vya awali. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

10. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba za usaili kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

12. Msailiwa haruhusiwi kuja na simu, saa au kifaa chochote cha kielekroniki kwenye eneo la usaili.

13. Ratiba ya Usaili inapatikana kupitia www.tra.go.tz Kwa taarifa Zaidi, tembelea Ofisi za TRA zilizo karibu nawe au tumia mawasiliano yafuatayo: Tovuti : www.tra.go.tz Namba za simu bila malipo : 0800 780078 au 0800750075 WhatsApp : 0744 23 33 33 Barua pepe : huduma@tra.go.tz au services@tra.go.tz ‘‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’’ Imetolewa na; Idara ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala.

 

DOWNLOAD PDF DOCUMENT