Loading...
company_logo

PDF YA WALIOITWA KAZINI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA (22-08-2023)

Aug. 22, 2023

TANGAZO

TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 07/01/2023, 01/03/2023, 05-20/02/2023, 12-15/05/2023 na 12-19/06/2023 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana. Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala yawazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta. Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Kwa Waombaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya, Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Fungua Link Hapo Chini.

Click To Download PDF

 

Kwa Waombaji Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Fungua Link Hapo Chini

Click To Download PDF