Loading...
company_logo

NAFASI (7) ZA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA MULEBA

Kagera full time

Job description

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI (LIMEONGEZWA MUDA WA KUTUMA MAOMBI)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba anawatangazia nafasi za kazi watanzania wote wenye sifa za kuajiriwa katika nafasi ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III. Hii ni kwa kuzingatia kibali cha Ajira Mbadala chenye Kumb. Na. FA. 170/368/01 "C"/71 cha tarehe 04/05/2023, na kibali cha Ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA.170/368/01 "C"/86 cha tarehe 10/07/2023 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Tangazo hili limeongezwa muda wa kutuma maombi kwa lengo la kukidhi takwa la Kanuni za Uendeshaji shughuli za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma za mwaka 2021, Sura ya 298, kuhusu Tangazo kuwekwa kwenye 'Website' ya Sekretarieti ya Ajira.
Waombaji ambao waliwasilisha maombi yao kwa kuzingatia tangazo lenye Kumb. Na. KGR/MLB/HW/A.225/VOL.V/34 la tarehe 11/8/2023, hawatakiwi kuomba kwa mara nyingine kwa sababu barua zao za maombi zilishapokelewa.

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III - NAFASI SABA (07)
SIFA ZA MWOMBAJI

1. Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
2. Awe amehitimu mafunzo katika ngazi ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo; Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii, na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

VIGEZO NA MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI.
1. Mwombaji awe raia wa Tanzania na umri kuanzia miaka 18 - 45.
2. Mwombaji awe hajawahi kushitakiwa kwa kosa lolote la jinai.
3. Waombaji wote waambatanishe nakala za vyeti vya taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha nne, na sita vilivyothibitishwa na Hakimu au Wakili anayetambulika na Serikali.
4. Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
5. Waombaji wote waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika, pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu (3) na picha moja ya "passport size" ya hivi karibuni (iandikwe majina kwa nyuma).
6. Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, Hati za matokeo za kidato cha nne na sita (Form IV and VI Results Slips) na Transcript ambayo haikuambatanishwa na cheti havitakubaliwa.
7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA au NACTE).
8. Waombaji ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma hawatakiwi kuomba nafasi hizi.
9. Waombaji watakaowasilisha vyeti, na taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria na mamlaka zinazohusika.
10.Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
11. Kwa waombaji wenye vyeti vya ngazi ya msingi yaani NTA Level 4 (Basic Technician Certificate), na ngazi ya stashahada NTA Level 6, maombi yao hayatashughulikiwa.
12. Waombaji wote waambatanishe nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), au Namba ya Utambulisho wa Uraia (National Identification Number) kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

13. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 11 Septemba 2023, saa 09:30 Alasiri.
14. Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo;

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA,
S. L. P 131,
MULEBA.

DOWNLOAD ATTACHED DOCUMENT

Job Summary

Published On: Sept. 8, 2023, 5:03 a.m.

Vacancy: 7

Job Nature: full time

Location: Kagera

Dead Line: Sept. 11, 2023

Company Detail

Muleba is one of the six districts of the Kagera Region of Tanzania. It is bordered to the north by Bukoba Urban and Bukoba Rural districts, to the south by Biharamulo District, to the east by Lake Victoria and to the west by Ngara and Karagwe districts. The district covers area of 3,518 square kilometres.