Loading...
company_logo

NAFASI MPYA (89) ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE

Temeke contract

Job description

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI (MKATABA MWAKA 1).
Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke inawatangazia nafasi za kazi( mkataba kwa mwaka mmoja) katika Hospitali na vituo vya Afya vifuatavyo:- Hospitali ya Mbagala Rangi tatu, Zahanati ya Sigara, Zahanati ya Sandali, Kituo cha afya Kijichi, Zahanati ya Kizuiani, Kituo cha Afya RoundTable, Kituo cha Afya Majimatitu, Zahanati ya Charambe, Zahanati ya Kilakala, Zahanati ya Kichemchem, Zahanati ya Chang'ombe, Zahanati ya Kigugi, Kituo cha Afya Buza, Kituo cha Afya Yombo Vituka, Zahanati ya Tandika, Zahanati ya Mikwambe, Zahanati ya Makangarawe, Zahanati ya Tambukareli, Zahanati ya Miburani, Zahanati ya Mzinga, Zahanati ya Toangoma, Zahanati ya Chamazi, Zahanati ya Mtoni na Zahanati ya Mbande Hivyo Watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi tajwa hapo chini watume maombi.

1. DAKTARI DARAJA II (Nafasi 2)

2. TABIBU DARAJA II (Nafasi 9)

3. MTEKNOLOJIA DARAJA II - RADIOGRAFA(MIONZI/RADIOLOJIA) (Nafasi 4)

4. MTEKNOLOJIA DARAJA II - RADIOGRAFA- ULTRA SOUND (Nafasi 6)

5. MTEKNOLOJIA DARAJA II - DAWA (Nafasi 11)

6. MTEKNOLOJIA MSAIDIZI - DAWA (Nafasi 4)

7. MTEKNOLOJIA MSAIDIZI -  MAABARA(Nafasi 1)

8. USTAWI WA JAMII DARAJA II (Nafasi 1)

9. AFISA MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA II (Nafasi 9)

10. MUUGUZI DARAJA II (Nafasi 28)

11. AFISA HESABU DARAJA LA II (ACCOUNTS OFFICER)(Nafasi 3)

12. MSADIZI WA AFYA - HEALTH ATTENDANTS (Nafasi 11)

" DOWNLOAD PDF DOCUMENT HERE "

Maombi yatumwe kwa : MKURUGENZI,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE,
S.L.P 46343,
DAR ES SALAAM.


Mwisho wa kutuma maombi,siku saba kuanzia tarehe ya Tangazo hili.


G. B. Mtisho Kny.MKURUGENZI WA MANISPAA
Kny: Mkurugenzi Mtendaji Manispaa Ya Temeke

 

Job Summary

Published On: Aug. 27, 2023, 9:31 a.m.

Vacancy: 89

Job Nature: contract

Location: Temeke

Dead Line: Aug. 30, 2023

Company Detail

Manispaa ya Temeke ni moja ya Halmashauri chache kongwe zenye utajiri na historia ambayo imechangia kuleta mabadiliko kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini. Kwa ujumla Temeke imekuwa kitovu cha upatikanaji wa uhuru wa Tanzania bara, pia kwa ukuaji wa michezo, utamaduni na maendeleo ya kilimo katika jiji la Dar es Salaam. Temeke ni moja ya Wilaya inayolibeba Jiji la Dar-es-Salaam, kivipi, Dar-es-Salaam ni Temeke kwa kuwa bandari ipo Temeke,viwanja vyote vya mipira kitaifa - Uwanja wa Taifa na uwanja wa Uhuru, pia ipo jirani na Uwanja wa ndege wa kimataifa, ni mwanzo wa Reli ya Tazara, ina Uwanja wa kimataifa wa maonesho - sabasaba, ina daraja la Nyerere ambalo ni la kimataifa. Samaki hupatikana kwa uwingi Temeke, ina fukwe nzuri za kuvutia zenye mchanga mweupe, ina wakazi wengi na wahamiaji wanaopata maeneo ya kujenga kutokana na kuwa na maeneo makubwa tena ya wazi.Ina mtandao mkubwa wa barabara za lami.hii ndiyoTemeke tunayoisema.