Loading...
company_logo

NAFASI 470 TAASISI MBALI MBALI ZA UMMA

Dodoma full time

Job description

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi mia nne sabini (470) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili

1.0 AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVESTOCK OFFICER II) - NAFASI 65

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyama (Animal Science) au Sayansi ya Kilimo waliobobea katika Sayansi ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au kutoka chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

2.0 AFISA MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA II (LIVESTOCK FIELD OFFICER II) NAFASI 210

SIFA ZA MWOMBAJI 

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma NTA Level 6) katika mojawapo ya fani zifuatazo:- Uzalishaji Mifugo; Uzalishaji Maziwa na Kuku; Afya ya Mifugo na Uzalishaji au Ukaguzi wa Nyama kutoka Vyuo vya Wakala wa Mafunzo ya Mifugo au kutoka chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

3.0 FUNDI SANIFU WA MAABARA ZA UVUVI DARAJA II (FISHERIES LABORATORY TECHNICIAN II) – NAFASI 6

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma NTA – level 6) katika mojawapo ya fani za Chemistry, Food Science and Technology,Fisheries Management and Technology, Fish Processing, Laboratory Technology,Aquaculture, Aquatic Science kutoka Vyuo vya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency – FETA) au kutoka vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

4.0 AFISA HABARI DARAJA LA II (INFORMATION OFFICER GRADE II) NAFASI 33

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu ya Uandishi wa Habari kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

5.0 MSAIDIZI WA MISITU DARAJA LA II - NAFASI 21

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) ya Misitu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

6.0 MSAIDIZI WA UVUVI - NAFASI 4

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI ambao wamepata mafunzo ya Uvuvi na kutunukiwa Astashahada ya Uvuvi (NTA Level 5) kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency – FETA) au kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

7.0 MPISHI II NAFASI 15

SIFA ZA MWOMBAJI

8.0 FUNDI SANIFU MIFUMO YA MAJI DARAJA LA II (PLUMBER) NAFASI 2

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi (FTC) katika fani ya mifumo ya maji na wenye uwezo wa kutumia Kompyuta.

9.0 MWANDAZI DARAJA LA II (WAITER) - NAFASI 4

SIFA ZA MWOMBAJI

Wenye cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV na kufuzu mafunzo si chini ya mwaka mmoja katikafani ya ‘Food and Bevarages’ yanayotolewa na chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

10.0 MTUNZA NYUMBA DARAJA LA II (HOUSEKEEPER) NAFASI 3

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI wenye Stashahada ya Home Economics au sifa inayolingana na hiyo kutoka kwenye Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. wenye

11.0 MHUDUMU WA JIKONI DARAJA LA II (KITCHEN ATTENDANT) – NAFASI 4

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne wenye cheti cha mafunzo ya Uhudumu wa Jikoni kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali..

12.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III (GAME WARDEN III) – NAFASI 4

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au cha VI wenye Astashahada ya awali ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali au; Wahitimu wa Kidato cha Nne au kidato cha Sita wenye Astashahada ya Uhifadhi Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

13.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II (GAME WARDEN II) – NAFASI 5

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au cha VI wenye Stashahada ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Diploma in Wildlife Management) kutoka chuo cha Wanyamapori na chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. 13.3 MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara ya Serikali yaani TGS C.

14.0 MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II (ACCOUNTS ASSISTANT II) - NAFASI 36

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali au cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.

15.0 AFISA MAENDELEO YA VIJANA DARAJA LA II (YOUTH DEVELOPMENT OFFICER II) - NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya Maendeleo ya Vijana kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

16.0 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III – NAFASI 30

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne wenye Astashahada ya Kilimo kutoka vyuovinavyotambuliwa na Serikali.

17.0 KATIBU WA KAMATI DARAJA LA II (COMMITEE CLERK)- NAFASI 10

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada /Stashahada ya Juu ya Sheria/Sanaa/ Utawala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

18.0 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 4

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

19.0 DAKTARI WA MIFUGO DARAJA LA II (VETERNARY OFFICER II) – NAFASI 10

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Tiba ya Wanyama (Veterinary Medicine) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) au kutoka Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali ambao wamesajiliwa na Baraza la Veterinari Tanzania.

20.0 AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT COMMUNITY DEVELOPMENT OFFICER) NAFASI - 2

SIFA ZA MWOMBAJI 

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au kidato cha sita, wenye Stashahada (Diploma) katika moja ya fani zifuatazo:- Maendeleo ya Jamii (Community Development), sayansi ya Jamii (Sociology), masomo ya Maendeleo (Development Studies), Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management), Jinsia na Maendeleo (Gender and Development), Rural Development kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

20.4 MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT) NAFASI -1

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au kidato cha sita waliohitimu mafunzo ya Astashahada katika mojawapo ya fani zifuatazo:- Elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, Ustawi wa Jamii, Saikolojia au fani nyingine zinazofanana na hizo kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.

Kusoma Maelezo Kamili Pakua PDF Hapo Chini

Download PDF Document

 

Job Summary

Published On: Sept. 5, 2023, 4:53 a.m.

Vacancy: 470

Job Nature: full time

Location: Dodoma

Dead Line: Sept. 10, 2023

Company Detail

The Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) is a government organ with a status of independent Department established specifically to facilitate the recruitment process of employees to the Public Service. Public Service Recruitment Secretariat was established by the Public Service Act No. 8 0f 2002 as amended by Act No. 18 of 2007, section 29(1).