Loading...
company_logo

NAFASI (20) ZA AJIRA HALMASHAURI YA MOSHI

Moshi full time

Job description

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa kuomba ajira ya Mtendaji wa Kijiji daraja la III, Dereva daraja la II na Msaidizi wa Kumbukumbu daraja la II na Mhudumu wa jikoni daraja la II. Tangazo hili ni baada ya kupokea Kibali cha ajira mbadala chenye Kumb Na. FA. 170/370/01 "B"/127 cha tarehe 24/07/2023 toka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.
Mchanganuo wa nafasi ni kama ifuatavyo -;


1. MTENDAJI KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 15)
1.1.SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne au Sita aliyepata mafunzo katika ngazi ya cheti ambae amejiimarisha katika fani zifuatazo:___
Awe na cheti cha Astashahada ya mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo- Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

 

2. DEREVA II NAFASI MBILI (02)
2.1.SIFA ZA MWOMBAJI
a) Awe na elimu ya Kidato cha nne
b) Awe na Leseni daraja C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali
c) Awe amehudhuria mafunzo ya Msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au NIT au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali
d) Waombaji wenye cheti cha majaribio ya ufundi daraja II na wenye cheti kuorodhesha viongozi (VIP) watafikiriwa kwanza
e) Awe na namba ya utambulisho wa Uraia kutoka mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).

 

3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II NAFASI MBILI (02)
3.1.SIFA ZA MWOMBAJI

Awe na elimu ya Kidato cha nne au sita mwenye stashada Kumbukumbu au NTA level 6 katika moja wapo ya fani zifuatazo: utunzaji wa kumbukumbu, urasimu Ramani (Carto graphy or Geonformstics) Sheria au kumbukumbu za Afya kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wenye ujuzi wa kompyuta

 

4. MHUDUMU WA JIKONI NAFASI MOJA (01).
4.1. SIFA ZA MWOMBAJI

a) Awe na cheti cha Kidato cha nne
b) Awe na cheti cha mafunzo ya mwaka mmoja au miwili katika mambo ya uandamizi/uhudumu wa jikoni.
c) Wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu watapewa kipaumbele.

 

5. MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
a) Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania
b) Waombaji wote wawe na umri kati ya miaka 18 hadi 45
c) Maombi yaambatishwe na vyeti vya taaluma, cheti cha kuzaliwa na Kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA, picha 2 (Passport size) za rangi za hivi karibuni
d) Hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (Testmonials Provisonal Results, Statement of results) hazitatambulika.
e) Kila mwombaji aambatanishe maelezo binafsi "CV" yenye anuani ya namba za simu na majina ya wadhamini
f) Waombaji wote waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe kuwa vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika ya TCU na NECTA
g) Maombi yote yatumwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI, HALMASHAURI YA WILAYA, S.L.P 3003,
MOSHI.


5.1. MWISHO WA KUTUMA MAOMBI
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17/09/2023 saa 9:30 Alasiri

DOWNLOAD PDF DOCUMENT

Job Summary

Published On: Sept. 7, 2023, 5:02 a.m.

Vacancy: 20

Job Nature: full time

Location: Moshi

Dead Line: Sept. 17, 2023

Company Detail

Moshi District Council was established in January, 1984 by provisions of section 8 and 9 of the Local Government (District Authorities) Act 1982 with 45 Councilors in Number, of which 27 were elected, 1 each from the Wards within the Council, 5 were elected by the Council from the persons nominated by party Organizations and 3 were appointed by the Minister .1 Member of Parliament represented the consistency (Moshi Rural) and 9 were elected by the Council from amongst the villages Chairmen.