Loading...
company_logo

PDF YA WANAOITWA KWENYE USAILI TANROADS

Sept. 14, 2023

TANGAZO

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), anawaalika waombaji wa nafasi mbalimbali zilizotangazwa katika Mikoa ya Singida na Tabora kwa ajili ya kufanya usaili wa Kuandika, Vitendo na Mahojiano uliopangwa kufanyika katika Mkoa wa Singida kuanzia tarehe 16 Septemba, 2023 hadi tarehe 18 Septemba, 2023. Usaili wa mchujo utafanyika katika Chuo cha Uhasibu Tanzania – Singida campus katika ukumbi wa NLT. Aidha, usaili wa mahojiano na vitendo utafanyika katika Ofisi ya TANROADS – Singida. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili utafanyika tarehe 16 Septemba, 2023 - 18 Septemba, 2023 kama inavyosomeka kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;

ii. Usaili wa Mchujo (kuandika) utafanyika tarehe 16 Septemba, 2023, Usaili wa Vitendo 17 Septemba, 2023 na Usaili wa Mahojiano utafanyika tarehe 18 Septemba, 2023.

iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, leseni ya udereva, Kitambulisho cha Uraia (NIDA), Hati ya kusafiria, au barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa.

v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;

vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, Hati za Matokeo za Kidato cha IV na VI (Form V and form VI Results Slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;

vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;

viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);

x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

xii. Mwombaji ambae hatakuwa na vigezo vilivyotajwa hapo juu atakuwa amejiondoa kwenye usaili huo.

 

DOWNLOAD PDF DOCUMENT