Loading...
company_logo

PDFs ZA WALIOTWA KWENYE INTERVIEW HALMASHAURI YA UBUNGO, CHATO, GEITA, UKEREWE, KALAMBO, LUDEWA NA KARATU

Sept. 2, 2023

TANGAZO

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI MBALI MBALI.

1. UBUNGO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo anawatangazia walioomba nafasi za ajira ya Mwandishi Mwendesha Ofisi daraja II na Msaidizi wa Kumbukumbu daraja II kwenye tangazo lililotolewa tarehe 14 Machi, 2023 lenye Kumb.Na. AB.113/388/95 Kuwa wamechaguliwa (Shortlisted) kuhudhuria usaili wa mchujo na Vitendo utakaofanyika kama ilivyoainishwa kwenye majedwali yafuatayo:-

Download PDF Document

2. CHATO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato anawatangazia walioomba nafasi za ajira ya udereva daraja II na Msaidizi wa Kumbukumbu daraja II kwenye tangazo lililotolewa tarehe 25 April, 2023 Kuwa wamechaguliwa (Shortlisted) kuhudhuria usaili wa mchujo na Vitendo utakaofanyika kama ilivyoainishwa :-

Download PDF Document

3. GEITA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita anapenda kuwatangazia kuwa waombaji kazi kwa kada ya Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II na Madereva Daraja la II kuwa usaili wa vitendo utafanyika tarehe 07/09/2023 saa 1: 30 Asubuhi na usaili wa mahojiano ya ana kwa ana utafanyika tarehe 08/09/2023 saa 1: 30 Asubuhi. Pia kwa waombaji kwa kada ya Mtunza Kumbukumbu Daraja la II usaili wa mchujo utafanyika tarehe 09/09/2023 saa 1:30 Asubuhi na usaili wa mahojiano ya ana kwa ana utafanyika tarehe 10/09/2023 saa 1: 30 Asubuhi. Eneo la usaili ni Ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita maeneo ya Geita Mjini.
Wasailiwa wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

Download PDF Document

4. UKEREWE

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe anawatangazia waombaji wa nafasi za kazi ya Dereva Daraja II, Mtendaji wa Kijiji Daraja lil na Mtunza Kumbukumbu Daraja II na Mwandishi mwendesha ofisi Daraja la II waliokidhi vigezo kutokana na Tangazo la ajira lenye Kumb. Na. GA.25/95/01/112 la tarehe 14/03/2023 na Kumb. Na. GA.25/95/01/112 la tarehe 21/04/2023 kuwa usaili unatarajiwa kufanyika tarehe 07/09/2023 hadi tarehe 10/09/2023 katika Ukumbi wa Uthibiti Ubora wa Shule, Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.
Watakaofaulu mtihani wa vitendo na mahojiano majina yao yatawekwa katika tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe (www.ukerewedc.go.tz) na yatabandikwa katika mbao za matangazo za Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.
Ratiba ya usaili kwa kada iliyotangazwa itakuwa kama ifuatavyo:-

Download PDF Document

5. KALAMBO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, anawatangazia waombaji wa nafasi za kazi waliotuma maombi kwa nafasi ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III, Dereva Daraja la II na Katibu Muhtasi Daraja III/ Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II kupitia Tangazo la kazi la tarehe 03.05.2023 mpaka tarehe 15.05.2023, kuwa utafanyika usahili wa kuandika,Mahijiano na vitendo kuanzia tarehe 07.09 2023 mpaka tarehe 11.09.2023 kuanzia saa 1:30 asubuhi katika Ofisi za Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kwa ratiba ifuatayo:

Download PDF Document

6. LUDEWA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa anapenda kuwatangazia waombaji wote walioomba ajira katika nafasi ya Dereva II, Katibu Mahsusi, Mtendaji wa Kijiji na Mtunza Kumbukumbu II zilizotangazwa kupitia tangazo la tarehe 07/03/2023 na tarehe 24/4/2023 kuwa usaili unatarajia kufanyika tarehe 07/09/2023 hadi tarehe 10/09/2023 saa 02:00 Asubuhi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.

Download PDF Document

7. KARATU

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Karatu anawatangazia waombaji wa Nafasi za Kazi waliotuma Maombi ya kuomba nafasi ya Dereva II, Mtendaji wa Kijiji III na II tarehe 31 Mei, 2023 kuwa Usaili utafanyika kuanzia tarehe 07 Septemba hadi tarehe 09 Septemba, 2023 kwa Madereva na kuanzia tarehe 09 Septemba hadi 10 Septemba, 2023 kwa Watendaji wa Vijiji.

Download PDF Document