Loading...
company_logo

TANGAZO LA KAZI KWA NAFASI YA RIGGER (5) EACOP PROJECT

Tanga full time

Job description

TANGAZO LA KAZI KWA NAFASI YA RIGGER

Mradi wa EACOP unahusisha ujenzi, uendeshaji, na matengenezo ya bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda mpaka Chongoleani Tanzania ambako kutajengwa gati na kituo cha kupakia mafuta ghafi karibu na bandari ya Tanga. BESIX Ballast Nedam (BBN) Limited, ni MKANDARASI anayehusika kwenye mambo ya uhandisi, ununuzi na ujenzi wa gati na kituo cha kupakia mafuta ghafi ya mradi wa EACOP. BBN inawatangazia wazawa wa kata ya Chongoleani kuomba nafasi ya kazi ya Rigger. (Msaidizi katika Mashine za Ushushaji na Upakiaji Mizigo).

Nafasi za kazi – 5

Mradi - EACOP – Jetty & Loading Out Facility

Muajiri - BESIX Ballast Nedam Limited (BBN)

Mahali - pakazi Tanga Nafasi ya kazi Rigger

Mkuu wa Idara: Meneja Ujenzi

Kipindi cha kazi - September 2023 – May 2025

Dhumuni la kazi

Jukumu kuu la Rigger ni kusaidia katika kuhamisha vitu vizito au mashine katika maeneo yanayotakiwa bila kusababisha uharibifu wa mzigo au mali inayosafirishwa au watu. Hii inajumuisha unyanyuaji na uhamishaji wa vifaa, kwakutumia mashine au visaidizi vingine huku ukizingatia kanuni na taratibu za usalama.

Jinsi ya kutuma maombi:

Anuani kwaajili ya maombi ya kazi ni: Meneja Mradi, BESIX Ballast Nedam Ltd. TANGA. Maombi yote yatapokelewa kupitia ofisi ya kata ya Chongoleani au barua pepe jobs@bbnltd.co.tz na mwisho wa kupokea maombi haya ni 10 Septemba 2023. Majina ya watu wote watakaofanikiwa yatabandikwa katika mbao za matangazo kwenye ofisi ya mtaa husika. Kwa maswali/maelekezo;- +255 747 958 460 (ndani ya muda wa kazi, saa 1:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni, Jumatatu hadi Jumamosi) ZINGATIA. Kwa nafasi hii, waombaji kutoka maeneo mengine ya Tanzania hawatakiwi kupiga muhuri barua zao za maombi katika Ofisi ya Kata ya Chongoleani, Ni wazawa wa kata ya Chongoleani wanaostahili kufanya hivyo.

Kusoma Taarifa Kamili Download PDF hapo chini:-

DOWNLOAD PDF DOCUMENT

Job Summary

Published On: Sept. 1, 2023, 4:24 p.m.

Vacancy: 5

Job Nature: full time

Location: Tanga

Dead Line: Sept. 10, 2023

Company Detail

Known for many years as an area where natural oil seepages occurred, oil was first discovered by drilling in the Lake Albert area of Uganda in 2006. This first discovery led to an extensive period of further exploration and appraisal which was completed in 2014. EACOP is being constructed in parallel with two upstream development projects which are not part of EACOP development and investment, known as Tilenga and Kingfisher respectively. Each development will consist of a Central Processing Facility (CPF) to separate and treat the oil, water and gas produced by the wells. Kingfisher will have 4 well pads and a CPF with a peak daily capacity of 42000 bbl/d. Tilenga has 31 wellpads and a 204000 bbl/d CPF.